Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye amewataka Watanzania hususani wana tasnia ya habari kuwa watulivu na kusubiri ripoti rasmi kuhusu tukio la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kile kinachoitwa kuwa ni uvamizi wa kituo cha matangazo cha Clouds Media kilichotokea siku ya Ijumaa.

Mapema leo akizungumza na kupitia Televisheni ya Clouds, Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Ruge Mutahaba ameeleza kusikitishwa na matumizi mabaya ya madaraka yaliyooneshwa na Mkuu huyo wa Mkoa.

Taarifa ya Mheshimiwa Makonda ziliibuliwa mwishoni mwa wiki baada ya video iliyokuwa ikitembea kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha mwanamke mmoja aliyedai kuzalishwa na mchungaji Josephat Gwajima huku akionekana mmoja wa watangazaji wa kituo hicho akifanya mahojiano na mwanamke huyo na baadaye kuibuliwa kwa video ya CCTV ikimuonesha Mkuu huyo wa Mkoa akiwa na askari waliokuwa na Silaha wakiingia ndani ya kituo hicho cha matangazo.