Akamatwa na Kete za Dawa za kulevya Bwejuu Mkoa wa Kusini Unguja

Msichana mmoja mkaazi wa Bwejuu Mkoa wa Kusini Unguja amekamatwa na dawa za kulevya  baada ya kufanyika doria na misako mbalimbali inayohusisha dawa za kulevya, bangi ,pombe za kienyeji.

Akithibitisha kukamatwa kwa msichana huyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi Suleiman Hassan Suleiman amesema mnamo 13-07-2018 majira ya saa 3:00  kamili usiku huko Bwejuu walimkamata msichana huyo.

Amemtaja msichana huyo kwa jina Aziza Ali Chovya (30) mshirazi wa Bwejuu akiwa na kete 84 za dawa za kulevya .

Kamanda Suleiman ameongeza kusema kuwa shauri hilo linaendelea na upelelezi ilikuweza kufikishwa mahakamani mara baada ya mtuhumiwa kuhojiwa na kupata ushahidi zaidi na utakapo kamilika zitafatwa taratibu za kisheria.

Aidha kamanda Suleiman ameitaka jamii kuridhika na kipato wanachopata na kuacha kujihusisha kwenye majanga hayo pamoja na kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuweza kuwachukulia hatua za kisheria  wale wote wanaojihusisha na majanga hayo ambayo visababishi vikubwa vinavyoharibu vizazi vyetu.

Rauhiya Mussa Shaaban