Wakati wiki hii ikielekea mwishoni na kukamilisha wiki nzima ,wiki hii tukio kubwa limetokea kwenye upande wa michezo Zanzibar na kupewa uzito kwenye vyombo vya habari na katika jamii ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla baada ya Mrajasi wa vyama vya michezo Zanzibar kuivunja kamati tendaji ya ZFA kwa kushindwa kuwajibika kikanuni na kudharau ombi la mrajisi la kutaka kutakiwa kurekekebisha baadhi ya vipengele kwenye katiba ya ZFA ya mwaka 2010 ambavyo vilikuwa vinaleta utata.

Hili limevuta sana hisia za watu wadau wa mpira wa miguu ndani na nje ya Zanzibar kwa kuona viongozi waliopewa dhamana ya mpira wa miguu Zanzibar kuwa wanawajibika kuondoka kwenye nafasi zao kwa kushindwa kuendesha mpira wa Zanzibar ambao unahitaji umakini katika kuuwendesha .

Maoni yetu ya wiki hii sisi dawati la michezo Zanzibar 24 ni kuungalia kuna haja kubwa ya mrajisi wa vyama vya michezo Zanzibar kurudi kwa vilabu vya Zanzibar hususani vile vya madaraja ya juu kwa Zanzibar yanayoendeshwa na ZFA Taifa kufanya mapitio ya kisheria na kikanuni ya vilabu hivi ili kundoa vikwazo vya mpira wa Zanzibar.

Watu wengi wamekuwa wakiona suala hili halina umuhimu kwa kuwa wanahisi ndani ya vilabu vyetu hakuna matatizo ya kikatiba kwa kuwa tunaikosoa sana katiba ya ZFA bila ya kungalia katiba za vilabu ambazo zinaonyesha wazi zinamapungufu ya kisheria.

Swala hili halihitaji ufafanuzi kwa muda mrefu vilabu vyetu vimekuwa na viongozi wanao jita maraisi wa vilabu na makatibu je katiba zao zinawatambua, wakati tunajipanga kurudisha mpira wa Zanzibar tusisahau vilabu ndio wadau wakubwa wa mpira wa Zanzibar.

Vilabu vyetu vimekuwa kwa muda mrefu havijafanya chaguzi za kuteuwa viongozi wapya wa kuendesha vilabu hivyo hususan hivi vilabu vya vikosi vya maaskari kwa muda mrefu viongozi wao huwa wale wale kinyume na taratibu za kuendesha mpira lazima turudi kwenye katiba zao kama zinamapungufu lazima zifanyiwe marekebisho haraka sana.

Tumekuwa na utitiri wa vilabu vingi Zanzibar lakini hatuoni mabadiliko ya uongozi kwenye vilabu hivyo na kuona viongozi wao wapo muda mrefu kinyume na taratibu za kuendesha mpira kwa mfumo wa kisasa mfano vilabu vilivyopoa kwenye madaraja ya ligi kuu ya Zanzibar Unguja na Pemba.

Umefika wakati sasa vilabu vya Vikosi (Majeshi) virudi uraiani hata ofisi zao za vilabu kwa kuwa tunataka mabadiliko ya mpira wa Zanzibar na wawe na katiba zinawafanya kufanya uchaguzi ndani ya vilabu vyao kwani wao ni vilabu vya mpira vilivyochini ya Ofisi ya mrajisi na Baraza la michezo pamoja na ZFA kama vilabu vyengine sasa lazima virudi kwa wananchi na kuhakikisha katiba zinapitiwa upya.

Maoni yetu tunaiomba sana ofisi ya mrajisi wa vyama vya michezo Zanzibar yenye mamlaka kisheria kupitia katiba za vilabu vyetu ili kuondoa vikwazo vinavyojitokeza kwa kuwa kuna baadhi ya wanachama wanahaki ya kutaka kuviongoza vilabu vyao pale wanapoona kuwa vilabu hivyo vinakwenda mrama kwenye masuala ya uendashaji wa michezo.

Taifa Jangombe moja ya vilabu vilivyofanya marekebisho ya katiba yao hivyo tunatarajia mabadiliko makubwa kwenye klabu yao na tunatarajia siku ya uchaguzi watapata viongozi madhubuti wa kuiyongoza klabu yao ya Taifa Jangombe .

Hatuna budi kumpongeza mrajisi wa vyama vya michezo kwa hatua kubwa alioichukua kwa kuivunja kamati tendaji ambayo haikuwa na meno wakati viongozi walipokuwa wakiboronga katika kuendesha mpira na kusimamia kanuni zilizopangwa hivyo panga hili lirudi kwa vilabu vyetu vingi vimekuwa na viongozi wa muda mrefu hawana malengo katika kuendesha vilabu vyetu.

Na: Ibrahim Makame Zanzibar24.