Ligi kuu ya Zanzibar hatua ya nane bora mzunguko wa Tano wa ligi kuu ya Zanzibar umemaliza kwa kupigwa michezo mbali mbali kwenye viwanja vya  Gombani na Amani Unguja .

Uwanja wa Gombani Pemba Zimamoto wamepokea kichapo cha goli moja kwa bila kutoka kwa KVZ ambao ndio wanashika nafasi ya pili ya ligi kuu ya Zanzibar wakiwa na alama saba, mchezo mwengine uliochezwa kisiwani Pemba Jamuhuri (wakombozi wa wete ) wamewalaza maafande wa Hardrock magoli mawili kwa bila.

Kwa upande wa kiwanja cha Uwanja wa Amani Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Zanzibar JKU SC  wametoka sare ya bila ya kufungana na maafande wa Mafunzo mchezo uliopigwa uwanja wa Amani mjini Unguja, mchezo mwengine ulikutanisha mafahari wawili klabu ya Mwenge baada ya kupokea kichapo dhidi ya Mafunzo mchezo wa mzunguko wa nne wamefanikiwa kundoka na alama tatu dhidi ya Opec na kurudi nafasi ya nne ya ligi kuu ya Zanzibar.

Msimamo wa ligi kuu ya Zanzibar kwa sasa unashikaliwa na klabu ya zimamoto wakiwa na alama 10 ,wakifuatiwa na Kvz wenye alama 7, nafasi ya tatu ikishikiliwa na Jku .

Ligi kuu ya zanzibar mzunguko wa Tano utandelea Alhamisi kwa kuchezwa michezo  minne kwa unguja na Pemba ,Kwa upande wa Unguja Kvz watacheza dhidi ya Opec na Zimamoto dhidi ya mwenge.

Kisiwani Pemba uwanja wa Gombani Hardrock dhidi ya Jku , na Mafunzo dhidi ya Jamuhuri.