Kamati teule inayosimamia ligi kuu ya Zanzibar na kuchukua nafasi ya ZFA imepata msemaji wa mpya wa kamati hiyo inayosimamia ligi kuu ya Zanzibar na mashindano yote ya ZFA.

Akithibitisha kuteuliwa kwake mwandishi wa Habari za michezo kutoka ZBC Abubakar Khatib Kisandu amesema kweli amepokea barua kutoka kwa Katibu msaidizi wa kamati hiyo Muhamed Hilali Tedy ya tarehe 7 mwezi Ogasti yenye namba ZFA/KM/141/VOL/4 kutoka ofisi ya ZFA Taifa.

Aidha Kisandu amekubali uteuzi huo na kuwaomba wadau wa michezo kumuunga mkono kwenye kipindi chote cha miezi sita ya utumishi wake ndani ya kamati teule hiyo kwa kuwa wapo kwenye kipindi cha kusimamia mpira wa Zanzibar.

Kwa Upande mwengine kisandu amewataka wandishi wenziwe wa michezo kuumpa ushirikiano kwa kuwa yupo katika majukumu mazito ya kitaifa ya kuusemea mpira wa Zanzibar ambao kimsingi umekuwa na Changamoto nyingi sana.

“Nafurahi uteuzi huu kwa kuwa ni mwanamichezo na muomba mungu anisaidie kwenye jukumu hili na nawaomba sana wandishi wa michezo na wandishi wote waniunge mkono sisi ndio wenye dhamana ya kufikisha mbali mpira wetu” Alisema Kisandu.

Abubakar Kisandu amengia kwenye orodha hii ya wateule wa jumbe na kubeba nafasi ya msemaji wa kamati hiyo teule, kabla ya hapo ZFA ilikuwa na msemaji Ali Bakari Cheupe.