Kimbunga Mangkhut chau 25 nchini Ufilipino na 13 watoweka

Kimbunga hicho kinacho julikanwa kwa jina la Mangkhut, kinachukuliwa kuwa chenye nguvu zaidi kuwahi kutokea eneo hilo mwaka huu, kikiwa na upepo unaosafiri Kilometa 200 kwa saa.

Kimbunga  Mangkhut kimeonekana kikipita katika Bahari ya Kusini mwa China kuelekea katika Jiji la Hong Kong na Pwani ya China.

Aidha, mapema leo asubuhi Mamlaka za Hong Kong zimeonesha ishara ya juu ya alama 10 ya dhoruba baada ya upepo mkali kuanza kupiga madirisha ya juu katika majengo marefu huku mawimbi ya bahari yakionekana kuongezeka nguvu.

Mamlaka ya anga pia imezuia safari zake katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hong Kong ili kujihami na Kimbunga hicho.