Ali Abdalla Ali mwenye umri wa miaka 22 mkaazi wa Pwani Mchangani amefariki dunia baada ya kuzama baharini wakati akiogelea huko Pwani Mchangani.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo la kuzama baharini Kamanda Haji Abdalla Haji amesema tukio hilo limetokea siku ya tarehe 14 ya mwezi huu majira ya saa 10:00 jioni huko pwani mchanagni wakati marehemu huyo alipoenda kuogelea na hatimae maji ya yameshinda na kusababisha kifo.

Kamanda Haji ametoa wito kwa wananchi wa maeneo ya fukwe wawe karibu na wageni wao wanaofika maeneo yao ilikuweza kujua kuwa wanajua kuogelea au hawajui na kuepusha vifo visivyo vya lazima.

Marehemu huyo amafanyiwa uchunguzi katika hospitali ya kivunge na baadae kukabidhiwa na jamaa zake kwa ajili ya mazishi .

RAUHIYA MUSSA SHAABAN