Madereva 37 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Kaskazini Unguja kwa tuhuma za kupandisha nauli na kutobandika stika za kiwango cha nauli kwenye gari zao.

Akizungumza na Hits fm radio Kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini Unguja Kamishna msaidizi wa polisi Haji Abdallah Haji amesema operesheni hiyo ya kukamata gari hizo imekuja mara baada ya malalamiko ya abiria wanaotumia gari hizo.

Katika tukio jengine kamanda Haji ameeleza kuwa kumetokea tukio la kuzama kwa mtu baharini huko Fukuchani na amepatikana akiwa ameshafariki tayari ameshakabidhiwa jamaa zake kwa ajili ya mazishi.

Hata hivyo Kamanda Haji ametoa wito kwa jamii kuwa makini katika kipindi hicho cha upepo na kuacha tatbia ya kwenda baharini mtu pekeyake ili kuepusha ajiali zisizo za lazima.

Rauhiya Mussa Shaaban