Jeshi la polisi mkoa wa kaskazini Pemba linawatafuta watuhumiwa wa kubaka na kunyonga kwa binti mmoja wa miaka 20  huko katika shehia ya Gando wilaya ya wete mkoani humo. 

Akizungumza na Zanzibar24 kamanda wa polisi kaskazini Pemba Hassan Nassir Ali alisema tukio hilo la kubakwa na kuuwawa kwa msichana huyo ambae ni (Salma Ally) ni la kwanza kwenye eneo hilo katika mwaka huu. 

Alisema  tukio hilo linasikitisha maana binti huyo alibakwa na kisha kuburuzwa katika fukwe za bahari  na badae waliofanya hivyo waliamua kumbena shingo na kupoteza uhai wake. 

Akieleza kuhusu mazingira ya kutoweka kwa binti huyo alisema jioni ya tarehe 7  aliondoka nyumbani kwao lakini muda mchache badae alirejea kama kawaida ila ilipofika majira ya saa kumi aliondoka tena na ndipo familia yake alipopata taarifa ya kuuwawa kwa binti yao majira ya tatu usiku. 

Aleleza kuwa wao kama polisi walipokea taarifa ya awali ilionesha ni kuwawa tu kwa mtu huyo lakini baada ya kufanya uchunguzi wao kwa kushirikiana na watalamu wa afya walibaini pia binti huyoo alibakwa na kasha ndio alinyongwa. 

Alieleza kuwa hadi sasa wameanza na hatua za kiupelelezi ili kuwabaini watuhumiwa waliofanya tukio hilo na kwa sasa tayari wemeanza kazi zao. 

Kamana Nassir alisema ili wahisika watukio hilo waweze kukamatwa ni lazima wananchi nao watoe ushirikiano wa kina kwa jeshi la polisi ili lilweze kufanya kazi zake kwa urahisi. 

Sambamba na hilo aliomba jamii kuacha kujihusisha na matendo ya aina hio alioyaita ya kinyama akidaikuwa yanaiharibu taaswira ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. 

Kwa upande wake Naibu waziri wizara ya kazi uwezeshaji wanawake na  watoto  Shadya Mohamed Suleiman alisema Zanzibar kwa sasa imekumbuwa na dimwit la udhalilishaji kila siku jambo ambalo limeanza kuleta hofu kwa wananchi wote. 

Sambamba na hilo alisema Serikali haitavumilia tukio hilo na itahakikisha kwamba wale wote waliofanya tukio hilo wanatiwa mkononi ili kufikishwa katika vyombo vya sheria. 

Aidha aliwataka wanafamilia ambao wamegiswana tukio hilo pamoja na jamii kwa ujumla kuendelea kuwa watulivu wakiamini kuwa wale wote waliohusia watapatikana haraka iwezekanavyo. 

Tukio hili la kubakwa na kuwawa kwa msichana huyu ni la pili katika kipindi kifupi baada ya lile la awali lililotokea wili tatu nyuma huko Tunguu mkoa wa kaskazini Unguja ambapo binti wa miaka 21 nae alibakwa na kunyongwa ambapo hadi sasa watuhumiwa wa tukio hilo wanaendelea kuhojiwa na jeshi la polisi mkoani humo. 

Baba Mzazi wa mtoto huyo Simai Ali , ameviomba vyombo vya ulinzi kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio la kifo cha mwanae . 

Amesema tukio hilo yeye hakuna mtu ambaye anamtuhumu kuhusika na kusema mwanawe alikuwako nyumban siku ya tukio majira ya jioni na kwamba taarifa ya kuokotwa ufukweni akiwa amekufa alizipata kutoka kwa wananchi. 

Alidai kuwa hafahamu lolote kwamba mtoto wake alingia kwenye ugomvi na mtu katika kipindi chote alichoishi nae hivyo anashangazwa sana na tukio hilo.