Chama cha ACT wazalendo kimemteua Bernard Membe kuwa Mshauri Mkuu wa chama hicho. Taarifa ya kiongozi wa chama, Zitto Kabwe imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza Agosti 2, 2020, na Membe atatekeleza majukumu yake kama yalivyoainishwa kwenye Katiba ya chama.