Hajra Abdallah Abdallah mwenye umri wa miaka 23 mkaazi wa paje amefariki dunia baada ya kudaiwa kuchomwa kitu chenye ncha kali katika maeneo tofauti ya mwili wake na mpenzi wake Haji Jaha Issa  huko Paje Mkoa wa Kusini Unguja .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Suleiman Hassan Suleiman amesema tukio hilo la kushambuliwa na kuchomwa kitu chenye ncha kali limetokea siku ya tarehe 26-02-2020 majira ya saa 9:10 Jioni huko Paje Mkoa wa Kusini Unguja.

Ameongeza kusema kuwa mtuhumiwa Haji Jaha Issa mwenye umri wa miaka 25 mkaazi wa paje ambae amemshambulia Hajra Abdallah Abdallah kwa kuchoma kitu chenye ncha kali katika sehemu ya kifua, tumboni pamoja na ubavuni na kusababisha kutokwa kwa damu nyingi na kupelekea kufariki dunia .

Mwili wa Marehemu ulipelekwa Hospitali ya Makunduchi na  kuhamishiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja kwa uchunguzi zaidi na kukabidhiwa jamaa zake kwa mazishi huko chanzo chake cha awali wivu wa mapenzi .

Mtuhumiwa wa tukio hilo bado anaendelea kutafutwa ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria  na kupelekwa mahakamani.

Nae Daktari katika Hospitali ya Cottage Makaunduchi ambae amepokea maiti hiyo Daktari Amour Muhusini amekiri kupokea maiti hiyo kutoka kwa jeshi la polisi waliiangalia maiti hiyo na ikisha kuipeleka hospitali ya mnazi mmoja kwa uchunguzi Zaidi .

Aidha daktari Amour amewataka wanajamii kupunguza hasira pindi pale panapotokea sitafahamu kwao kwani kufanya hivyo kunaweza kuleta matatizo kwao na baada yake kusuhulishana katika familia zao.

Rauhiya Mussa Shaaban