Baada ya Elizabeth Michael (Lulu) kuhukumiwa miaka 2 jela kwa kosa la kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba. Msanii Afande Sele aliibuka na kuandika ujumbe wa kumshtumu marehemu Kanumba kwa kitendo cha kutembea na Lulu wakati akiwa bado mdogo na kueleeza kuwa ameumia zaidi baada ya matatizo aliyoyapata Lulu kupitia Kanumba, hivyo hakushiriki kivyovyote katika msiba wa msanii huyo ingawa alikuwepo Dar kwani hakutaka kuvaa joho la unafki.

Sasa leo hii Msanii Mrisho mpoto ameiibuka na kupinga vikali kile alichoandika Afande Sele, kupitia ukurasa wake wa Instagram Afande Sele ameandika yafuatayo;

Kaka yangu Afande Sele.. Mfalme wa maandishi…!! @afandeselekingWewe ni Kaka yangu na ni mwandishi ambae sijawahi kuacha kuheshimu maandishi yako …Leo nna mambo kadhaa kidogo kwako Kaka yangu…. Nimesoma maandishi kwenye ukurasa wako zaidi ya mara 30 Huku nikiyarudia rudia mara Kadhaa…ningependa kujua vitu Vichache kabla ya hoja yangu ya msingi kuiweka mezani…ile Barua ulimwandikia Marehemu Kanumba ulitaka imfikie? Au ulitaka wanaokwenda nyuma yake wamfikishie? ulitaka waliopo wajifunze kupitia walaka wako? Mbona nimepata kusikia Marehemu huwa halaumiwi kwakua hana uwezo wa kijitetea? Umesema ulikuwepo Sinza wakati wa msiba na hukutaka kusogea wala kuzika kwakua unasema wewe siyo mnafiki kama watanzania waliokwenda kuzika… ikiwa watu wote wangekataa ile Maiti ingekuaje? Nini Hasa lengo la Movies za Kibonge kuziita Maigizo yanayowekwa Kwenye Kanda? una ugomvi na Bongo Movies au uliandika ukiwa kwenye Jazbda kidogo….!! Mimi ndugu Mrisho Mpoto