Mwanaume mmoja katika kijiji cha Gionsaria,kaunti ya Kisii Nchini Kenya amefariki dunia baada ya mwanamke mmoja kumbana /kufungia kichwa cha mwanaume huyo katikati ya mapaja. 

Tukio hilo limetokea siku ya Ijumaa Disemba 28,2018, Chifu wa eneo hilo Oganda Matego amesema mwanaume huyo anayejulikana sana kwa jina ‘Doctor’,ambaye pia ni taniboi wa magari ya kusafirisha majani ya chai eneo hilo, alibanwa kichwa chake katikati ya mapaja/miguu na mwanamke mmoja.

Amesema wakati mwanamke huyo akiwa amebana kichwa cha mwanaume katikati ya mapaja, rafiki wa mwanamke huyo ambaye pia ni mwanamke alikuwa ameshikilia miguu ya ‘Doctor’na kumuinua hewani/juu.

Oganda amesema inashukiwa kuwa wawili hao walikuwa wapenzi na kifo cha ‘Doctor’ kilitokea wakicheza ambapo baada ya dakika moja mwanaume aliachilia kichwa na kubamiza kichwa kwenye barabara ya lami. 
Inaelezwa kuwa wanawake hao walimpeleka ‘Doctor’ katika hospitali ya wilaya ya Nyamache na madaktari walipompima wakabaini kuwa tayari alikuwa amefariki dunia.

Tayari wanawake hao wanashikiliwa na polisi kwenye kituo cha polisi cha Nyangusu huku wakisubiri kufunguliwa mashtaka.

Aidha baada ya habari ya kifo cha ‘Doctor’ kuwafikia majirani wa wanawake hao,waliamua kuchoma nyumba nne zinazomilikiwa na hao wanawake. 

Hali ya utulivu imeshuhudiwa kwa sasa na Chifu wa eneo hilo Oganda Matego amewasihi wakazi wa eneo hilo kutochukua sheria mikononi mwao kiholela.