Mtu mmoja ametambulika kwa jina Mudathir Khamis Omar (15) mshirazi wa Unguja Ukuu amefariki dunia baada ya kugongwa na gari huko Unguja Ukuu chimbechimbe Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja  .

Akithibitisha kutokea Kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Suleiman Hassan Suleiman amesema kuwa mnamo tarehe 17-09-2018 majira ya saa 12:30 jioni huko Unguja ukuu chimbechimbe imetokea ajali Ya gari kumgonga mpanda baskeli na kufariki dunia .

Ameongeza kusema kuwa ajali ilihusisha gari aina ya Excell yenye namba za usajili Z 175 GC iliyokuwa ikiendeshwa na Dereva Luic Clarence Peter iliyokuwa ikitokea Pete kuelekea Kikungwi.

Kamanda Suleiman amemtaja marehemu huyo kuwa ni Mudathir Khamis Omar (15) mshirazi wa Unguja Ukuu chimbechimbe aligongwa na gari hiyo wakati mpanda baskeli huyo akikatisha barabara.

Marehemu huyo alipata maumivi makali na kufariki dunia wakati akikimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu hadi tunatuma Habar hii marehemu huyo yuko chumba cha kuhifadhia maiti hosptali ya Mnazi Mmoja .

Kamanda Suleiman ametoa wito Kwa madereva kuheshimu sheria za barabara ilikuepuka ajali ambazo zinaweza kuepukika na pia kuwaheshimu waendao na vyombo vyengine ili kuepusha athari nyengine.

Rauhiya Mussa Shaaban