Masheha wametakiwa kulipa umuhimu suala la uhaulishaji wa ardhi ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza katika maeneo yao.

Wito huo umetolewa na afisa mtambuzi wa ardhi kutoka kamisheni ya ardhi zanzibar Shawana Soud Khamis wakati alipokuwa akitoa mafunzo kwa masheha 21 wa wilaya hiyo mafunzo ambayo yamefanyika huko makunduchi.

Amesema iwapoa masheha watasimamia ipasavyo majukumu yao katika uhaulishaji wa ardhi wataweza kupunguza kesi za wananchi kuuziana ardhi kiholela.

Amefahamisha kuwa kuna baadhi ya wananchi wanauza ardhi kwa wageni bila kufuatavutaratibu wa serikali na kupelekea baadhi ya wageni hao kuanzisha miradi kwa maslahi yao nbunafsi na kuikosesha serikali mapato.

Aidha amesema kuna baadhi ya watu hawaendi kuripoti kuripoti kwa masheha wakati wanapouziana jambo ambalo linasababisha masheha kukosa kumbukumbu sahihi na kushindwa kutoa maamuzi wakati yanapotokezea matatizo.

Kwa upande wake mwanasheria kutoka bodi ya uhaulishaji Wa ardhi Zanzibar masoud salum hemed amewataka wananchi kufuata taratibu Na sheria za uhaukishaji Wa ardhi ili kunusuru athari zinazoweza kujitokeza katika maeneo yao.

Nao masheha hao wamesema wanakabiliwa na tatizo la wananchi kutoripoti kwa masheha wakati wanapouziana ardhi na badala yake wanasubiri yanapotokezea matatizo jambo linawapa usumbufu mkubwa Wa kutatua migogoro hiyo.

Hata hivyo wameahidi kuchukua juhudi za makusudi zitakazohakikisha wanaifikisha elimu hiyo kwa vijana ili kuondosha migigiro ya adhi katika wilaya hiyo.