Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara imempiga faini ya shilingi laki mbili Beki wa Timu ya Azam FC Agrey Moris kwa kosa la kugoma kuongea na waandishi wa habari mara baada ya mchezo kumalizika katika mechi baina ya Timu yake na Polisi katika mchezo uliopigwa Februari 5.

Taarifa ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa Vyombo vya Habari leo imesema kwamba adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni namba 38(18) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.