Mkazi wa Kijiji cha Nange Mkoani Mwanza, Shabo Marando mwenye umri wa miaka 47 amehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kumbaka Bibi wa miaka 60.

Hukumu hiyo imetolewa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza Esther Malick baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka uliokuwa na Mashahidi wanne.

Shahidi wa tatu Dkt Judith Kiwango wa Hospitali ya Wilaya hiyo amesema baada ya kumfanyia uchunguzi Bibi alimkuta na michubuko sehemu za siri na manii, Shahidi wa Pili Sama Luheka amesema alisikia kelele kichakani aliposogea alimkuta Mtuhumiwa akimbaka Bibi.

Bibi huyo ameiambia Mahakama kuwa siku ya tukio Mtuhumiwa alimkuta shambani akikusanya kuni akamkamata kwa nguvu na kumvutia kichakani kisha kumbaka.