Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Njombe imemuhukumu kifungo cha maisha jela mtuhumiwa Addo Aron Nziku mwenye umri wa miaka 26, baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 8 katika Kijiji cha kitulia, Njombe.

Mtuhumiwa anadaiwa kumuingilia Mtoto huyo zaidi ya mara tatu kabla ya Mtoto huyo kumueleza Bibi yake anachofanyiwa.

Addo Nziku alimfanyia kitendo hicho Mtoto mara 3 katika eneo moja nyuma ya nyumba ya Wazazi wa Mtoto na siku nyingine katika eneo la kukata majani ya mifugo ambako mtoto huyo alitumwa kwenda kukata majani .

Mahakama imemtia hatiani Mtuhumiwa baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa kwa kumkuta na hatia ya kubaka kinyume na kifungu cha Sheria namba 130 kifungu kidogo cha kwanza na cha pili E  sambamba na kifungu namba 131 kifungu kidogo cha tatu cha kanuni ya adhabu namba 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.