Shabiki wa club ya Birmgham City Paul Mitchell mwenye umri wa miaka 27 apelekwa jela kwa kipindi cha miezi 14 na faini ya pound 35o pamoja na kufungiwa kwa miaka 10kuingia uwanjani kuangalia mechi yoyote katika ardhi ya UK kwa kumshambulia staa wa Aston Villa Jack Grealish wakati wa mchezo wa Championship kati ya Birmgham City dhidi ya Aston Villa uliyomalizika kwa Aston Villa kushinda 1-0 wakati wa mchezo huo kwa kuingia uwanjani.

Kufuatia tukio hilo kujitokeza na tukio la shabiki mwingine kuonekana akiingia uwanjani wakati wa mchezo wa Arsenal dhidi ya Man United, chama cha soka England FA kimetangaza kuongeza ulinzi kwa wachezaji na waamuzi wakati wa michezo mbalimbali sambamba na kufanya kazi na taasisi nyingine binafsi ambazo zitasaidia kulinda usalama wa wachezaji.