Mahakama katika mkoa wa Liaoning, kaskazini mashariki mwa China imehukumu mwanaume mmoja kifo kwa kuua watoto 6 na kujeruhi watu wengine 20 baada ya kuwagonga na gari kwa makusudi walipokuwa wakivuka barabara.

Mtuhumiwa, Han Jihua, aliendesha gari ndogo ndani ya kundi la wanafunzi 60 pamoja na walimu wao kabla ya kutoroka baada ya kusababisha mauaji hayo.

Mahakama hiyo imesema kwamba mtuhumiwa alitenda kosa hilo kwa makusudi na kudai kwamba alikuwa akipitia hali ngumu ya kifedha na familia yake.