Mwanaume mmoja amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mnazimmoja baada ya kupata ajali ya kugongwa na gari akiwa amepanda Pikipiki na kuumia vibaya sehemu ya Kichwa.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Suleiman Hassan Suleiman amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 3: 45 asubuhi huko Kidimni wilaya ya Kati Unguja huku akimtaja marehemu huyo kuwa ni Salum Kitwana Salum.

Amesema gari iliyomgonga ni ya abiria yenye namba za usajili Z 436 HT Iliyokuwa ikiendeshwa na Sleyum Salum Sleyum akitokea Dunga kuelekea Miwani.

Kamanda Suleiman ametoa wito kwa madereva kuwa waangalifu wanapoendesha vyombo vya moto kwani barabara hutumiwa na watu mbalimbali wakiwemo waenda kwa miguu,Wazee, watoto na wanyama.