Jeshi la Polisi Mkoani Mara limemkamata Juma Wambura kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kumchoma na kisu sehemu mbalimbali za mwili, kisha na yeye kujijeruhi

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Daniel Shillah amesema baada ya kupata taarifa, walifika Kijiji cha Nyamakango, Wilayani Butiama alipojificha Wambura lakini kabla ya kumuweka chini ya ulinzi, alijaribu kujiua kwa kujichoma na kisu tumboni

Shillah amenukuliwa akisema, “Aliposikia kuwa Polisi wanaelekea alipo alijaribu kujiua kwa kujichoma na kisu mara kadhaa tumboni lakini Polisi waliweza kufika na kumkamata ingawa tayari alikuwa ameshajijeruhi ”
Mtuhumiwa huyo alikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mara na anasubiriwa apone ili afikishwe Mahakamani kujibu shtaka la mauaji