Watu wanne wamefariki katika matukio tofauti Mkoani Rukwa, likiwemo tukio la Rafael Leonard (49) kujinyonga kwa kutumia kamba baada ya kugundua mke wake amemtoroka usiku na kwenda kwa mwanaume mwingine

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Justine Masejo, alisema kabla ya kujinyonga, Rafael alikuwa amelala na mkewe na aliposhtuka usingizini alikuta mke wake ametoroka na kwenda kwa mwanaume mwingine ndipo alipokasirika na kupatwa na wivu wa kimapenzi na kuamua kujinyonga

Katika tukio la pili, watu wawili waliofahamika kwa majina ya Japhet Jelazi (25) na Peter Silunde (8) walifariki papo hapo baada ya kupigwa na radi wakiwa wamejikinga mvua chini ya mti

Katika tukio la mwisho lililotokea katika Kitongoji cha Milundikwa, mtoto Emiliana Kauzeni (3) alikufa maji baada ya kutumbukia kwenye dimbwi la maji yaliyokuwa yametuama nyuma ya nyumba yao kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo