Akamatwa akiwa na shehena ya dawa za kulevya Nungwi

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Kaskazini Unguja Linaendelea Kufanya Doria Mbali Mbali Inayohusu Dawa Za Kulevya, Pombe Za Kieneyeji Na Makosa Mengineyo kwa lengo La Kupunguza Vitendo Vya Uhalifu Katika Mkoa Huo .

Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Kaskazini Unguja Kamishna Msaidizi Muandamizi Haji Abdala Haji Amesema Mnamo Tarehe  8 Januari 2019 Majira Ya Saa 6 :15 Mchana Huko Nungwi Mkoa Wa kaskazini Unguja Wamemkamata kijana Khamis Hassan Makame (24)  Mkaazi Wa Kwalinatu Akiwa Na Busita 10 Sawa Na  Kete 1197 Za dawa za Kulevya.

Kamanda Haji Ameeleza  Kuhusiana Na Doria Hiyo Inayofanyika Katika Maeneo Hayo Ya Kiwengwa Pwani Mchangani Na Kwengineko Ikiwa  Na Lengo La Kulinda Utalii Katika Maeneo Hayo .

Sambamba Na Hayo Kamanda Haji Ametoa Wito Kwa Jamii Kushirikiana Na Jeshi La Polisi kuwapatia Taarifa Zinazohusu Dawa Za Kulevya Ili kuzifanyia Kazi Na Kuwataka Kupinga Vita Dawa Za Kulevya Katika Maeneo Yao.

Rauhiya Mussa Shaaban