Akaunti zote rasmi za mitandao ya kijamiii ya rais wa Kenya Uhuru zimefungwa baada ya kutumiwa na watu ambao ”hawajaidhinishwa”, amesema mkuu wa wafanyakazi wake kwenye ujumbe wa Twitter.

Nzioka Waita hakutoa taafa kuhusu namna uingiliwaji wa mitandao hiyo ulivyotokea, lakini akaongeza kuwa itarejeshwa tena mtandaoni baada ya kuchukuliwa kwa “hatua za suluhu ya tatizo hilo “.

Ujumbe wa Twitter wa @NziokaWaita: On account of unauthorized access to the official social media handles of H.E the President of the Republic of Kenya, Uhuru Kenyatta .All official social media handles for the President have been temporarily suspended to allow for the necessary remedial measures to be undertaken.

Akaunti za Twitter na Facebook za Bwana Kenyatta zina mamilioni ya wafuasi.T

Gazeti la kibinafsi la The Star nchini humo limeripoti kuwa ujumbe uliotumwa kwenye Twitter unaoangaliwa kama kuwa nwenye utata wa kisiasa, uliotumwa leo asubuhi, ulikuwa ndio sababu ya kufungwa kwa akaunti hizo.

Chanzo BBC Swahili.