Mjumbe wa Baraza la Wazee Yanga, Ibrahim Akilimali amesema anatamani kuona tarehe 5 Mei inafika haraka ili uchaguzi mkuu wa klabu hiyo ufanyike.

Yanga itafanya uchaguzi wake mkuu mei 5 ili kupata viongozi wake wapya ambao wataongoza kwa muda wa miaka minne ijayo.

Akilimali amesema amekuwa na uchu wa kuiona Yanga inafanikiwa kupata viongozi wapya kwani imekaa muda mrefu bila kuwa na uongozi.

Ameeleza anatamani tarehe 5 ifike haraka ili naye akapige kura yake kwani ni haki yake na amejinadi lazima akapige kwa kiongozi ambaye kwake anaamini ataleta mabadiliko Yanga.

Aidha, Akilimali amewataka wanachama wa Yanga kuhakikisha wanachagua kiongozi makini na mwenye sifa nzuri za kuiongoza klabu yao ili ifike mbali kimaendeleo.