Akiona cha moto baada ya kumpiga jiwe la kichwa mkewe na kumuua

Mfanyakazi wa Kampuni ya simu TTCL mkoa wa Shinyanga aitwae Bupe Jacob maarufu kwa jina la Mwakibibi (48) ameuawa kwa kupigwa jiwe kichwani na mume wake aitwaye Shyrock Kimaro (48) mwendesha bodaboda mkazi wa Ibadakuli mjini Shinyanga.
Kwa Mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ,ACP Alchelaus Mutalemwa tukio hilo limetokea Novemba 5,2018 majira ya saa 12 jioni katika Mtaa Miti Mirefu kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga.
Amesema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi baina ya Shyrock na mkewe Bupe ambao walitengana hivi karibuni.
 
“Siku ya tukio Bupe alimpigia simu mme wake akiomba pesa za matumizi ya mtoto lakini simu haikupokelewa,na baada ya mme kuona missed calls nyingi akamfuata mwanamke,wakaanza kujibizana na kusukumana, Bupe akaaanguka chini mme aliyekuwa amelewa akachukua jiwe na kumpiga mkewe kichwani,akafariki dunia”,amesema Kamanda Mutalemwa.
Amesema tayari jeshi la polisi linamshikilia mtuhumiwa na atafikishwa mahakamani.