Algeria inakabiliwa na mgogoro wa kiuchumi kutokana na kushuka kwa kasi kwa pato linalotokana na mafuta, ambayo ni chanzo kikuu cha kiuchumi cha nchi hiyo.

Waziri wa Fedha wa Algeria Mohammad Loukal amelionya baraza la juu ya bunge la nchi hiyo kuharibu zaidi hali ya akiba ya fedha za kigeni na nakisi ya bajeti, ambavyo vimeitatiza sana serikali ya nchi hiyo tangu mwaka 2014 wakati bei ya mafuta duniani iliposhuka kwa kasi.

Amesema serikali ililazimika kutumia akiba ya fedha za kigeni kutoka dola za kimarekani bilioni 200 mwaka 2014 hadi bilioni 70 mwaka huu ili kuondoa nakisi katika bajeti ya fedha ya mwaka.