Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro amezungumzia suala la Viongozi wa CHADEMA kusema wanatishiwa maisha akisema aliiandikia barua CHADEMA kuomba Tundu Lissu aende kusema anatishiwa na nani

IGP Sirro amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ndogo ya Jeshi hilo jiji Dar es salaam kuhusu idadi ya watu waliyofariki katika matukio ya uchaguzi Zanzibar.

“Wakati ndugu yetu Tundu Lissu (Aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema) alipokwenda ubalozini akisema anatishiwa , niliandika barua aje basi atuambie anatishiwa na nani, lakini habari ya kutishiwa wewe unaweza ukagombana na mtu akakutishia, kama umetishiwa unatoa taarifa polisi,”– IGP Sirro

“Jeshi la Polisi lilimuita mara kwa mara Tundu Lissu aje atoe ushirikiano juu ya tukio lake la kupigwa risasi kule Dodoma, lakini hakutaka kufanya hivyo anapolisema Jeshi la Polisi linamuonea hii siyo sawa” IGP Sirro

“Tanzania tuko salama, niwaambie tena Tundu lissutz na Godbless_lema na wengine waliokimbia nchi warudi, Tanzania iko salama waje tujenge nchi”– IGP Sirro.