Alikiba afunguka wasanii walio mfuata Director wake

Msanii wa muziki wa kizazi kipya  Alikiba amefunguka kuhusu baadhi ya wasanii kumpigia simu Director wa wimbo wa Toto kwa ajili ya kuyataka material ya wimbo huo.

Kiba amesema hayo wakati anafanya mahojiano na kipindi cha Playlist kinachoruka Timesfm baada ya kuulizwa, kuwa kuna baadhi ya wasanii walisemekana kumpigia simu director wa Toto ni kweli?

 ” Ni kweli kuna watu walimpigia simu Director ni kitu cha ajabu sana na sikufurahishwa nacho, kwanza sio mara ya kwanza kuna director niliwahi kugombana nae na tukaacha kufanya kazi naye kisa aliwapa watu fulani material ya wimbo wangu” alijibu Alikiba

” Wanachukua nyimbo zangu wanasikiliza sijui wanataka nini na najua kuna sehemu fulani wamechukua wimbo wangu fulani na hiki kitu kinaniumiza sana sipendezwi nacho kabisa, nampongeza sana Manwalter kwani hajawahi kumpa mtu yoyote wimbo wa mtu mwingine aisikilize yuko profesional sana, kwani hawezi kutoa material ya mtu hata umpe nini” aliongezea kusema