Alikiba amfariji Ommy Dimpoz kwa staili hii

Ikiwa Leo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Msanii Ommy Dimpoz,  Ali Kiba ambaye ndie mtu wake wa karibu amemtumia ujumbe wa kumtakia Kheri katika maisha yake.

Ali Kiba ameandika Ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kumtaka Ommy Dimpoz
akazane na aamini kuwa Mungu ana maana yake na ndie Muumbaji wa Wanyonge na Wajanja hivyo anapaswa kumshukuru.

“Happy Birthday @ommydimpoz enjoy your special day bro Na wala Usiwaze.Mwenyezi Mungu ndie Muumbaji Wa wanyonge Na wajanja . Hivyo basi tunatakiwa tumshukuru kwa kutupa/Na Kutunusuru kwasababu Mungu Ana maana yake na anatupenda Sote ..KAZA 💪🏾
#mofayabyalikiba #KingKiba”