Alikiba na Diamond sasa mambo safi

Msanii wa Muziki Bongo Alikiba  amejibu Kauli ya Diamond Platnumz aliyedai yupo tayari kumshirikisha msanii huyo katika tamasha la la Wasafi Festival.

” Hili tamasha ni lakwetu sote kwa wasanii wote wa Kitanzania na katika tamasha hili ningefurahi sana kama kaka yangu Alikiba atakuwepo kwenye Tamasha hili” alisema Diamond Jana Novemba 5, wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika uzinduzi wa tamasha la Wasafi Festival 2018 jijini Dar es Salaam.

Diamond Platnumz kutangaza kuwa anatamani sana kumuona msanii mwenzake pia akiwa kama kaka yake kwenye muziki Alikiba awepo kwenye tamasha lake la Wasafi Festival ambalo linatarajiwa kuanzishwa mwezi wa 11 tarehe 24 mwaka huu ambalo linatarajiwa kuanzia mkoani Mtwara.

Usiku wa kuamkia leo Alikiba alipost kwenye ukurasa wake wa Instagram picha ya mchekeshaji maarufu sana kutoka Marekani Mr Benn, ambayo inasomeka ” Thank you for listerning to my presentation”

halafu chini ya post hiyo akaandika “Your welcome”

 

Je kwa post hii na hichi alichokiandika inamaanisha kuwa Alikiba amekubaliana na ombi hili la Diamond ?