Ria mmoja wa Marekani mwenye asili ya Tanzania anayedaiwa kuingia nchini wiki nne zilizopita akimtuhumu kukwepa karantini ya siku 14 amekamatwa huko mkoani dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi amesema Serikali lazima ifanye uchunguzi dhidi ya raia huyo na hivyo amemuweka chini ya uangalizi wa timu ya wataalamu wa afya kwa ajili ya uchunguzi.

“Alijitetea kuwa alijiweka karantini siku 14 nyumbani kwao, lakini hatuwezi kuyaamini maneno yake, hivyo lazima wataalamu wa afya wamchunguze,” alisema Katambi.