Aliekuwa Mgombea wa Ujumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mnara wa Voda, UngaLimited Arusha kupitia CHADEMA kabla ya Chama hicho kujitoa, Sirili ‘Rasta’ amekutwa amefariki kwa madai ya kuchinjwa nyumbani kwake.

Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha Jonathan Shana amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

“Bado tunachunguza maana Mtu amekutwa ndani na funguo ikiwa ndani inawezekana amejidhuru mwenyewe kutokana na labda msongo wa mawazo” amesema.

RPC Shana ameendelea kwa kusema, “Kuna Wanasiasa wanaoleta uchochezi kuhusu kifo hiki wakiendelea tutawachukulia hatua kwa mujibu wa Sheria, watuache tufanye kazi watupe muda tutatoa taarifa.