Aliyekuwa mwenyekiti UVCCM taifa John Guninita amefariki dunia

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM), Taifa na baadaye akawa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita amefariki dunia Alfajiri ya leo Septemba 13, 2018 alipokuwa amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili  akipatiwa matibabu.

Mdogo wa marehemu Gerald Guninita aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilolo wakati wa Uongozi wa Awamu ya Nne ndie aliyethibitisha taarifa za kifo cha kaka yake John Guninita.