Leo tarehe 11 Februari Serikali imekamilisha upelelezi wa kesi ya kufanya ngono kinyume na maumbile inayomkabili msanii Rutyfiya Aboubakary ‘Amber Ruth’ na mumewe Said Mtopali kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. 

Wakili wa Serikali, ameeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Augustine Rwizile.

Wakili Nguka amedai kuwa, upelelezi wa kesi hiyo , hivyo wanaomba tarehe kwa ajili ya kumsomea maelezo ya awali.


Baada ya kueleza hayo, Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 7 Machi 2019.


Amber Ruth na mumewe walifikishwa mahakamani hapo tarehe 2 Novemba 2018 wakikabiliwa na kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile.


Katika kesi hiyo kosa la kufanya ngono kinyume cha maumbile linamkabili Amber Ruth, ambapo anadaiwa ametenda kati ama baada ya tarehe 25 Oktoba 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary kumuingilia kinyume na maumbile, kosa ambalo amelikana.