Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Anthony Asenga (33), mkazi wa Kijiji cha Mrere wilayani Rombo anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kutenganisha kiwiliwili na kichwa cha Happiness Sianga aliyekuwa na ujauzito unaokadiriwa kuwa wa miezi nane

Tukio limetokea usiku wa kuamkia Februari 12 na kisha mtuhumiwa alijisalimisha Kituo cha Polisi cha Mashati

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Sembalo, Faustina Urassa alisema wanandoa hao waliwahi kugombana na kutengana kwa muda mrefu na siku ambayo tukio limetokea ndiyo waliyopatana na kuanza kuishi tena pamoja

Alisema kifo hicho kimeacha maswali kwa jamii kwa kuwa walitarajia kupata mtoto baada ya kurudiana na hivyo amani ingerejea katika familia yao