Novemba 18 pale Setsoto , Lesotho huenda ikawa siku ya kihistoria kwa Watanzania na inshallah siku hiyo iwe ya kheri ambapo Taifa Stars wakiwa na Milioni 50 walizokabidhiwa na Rais Magufuli kazi yao itakuwa moja tu , ushindi dhidi ya lesotho.

 

Kutimiza hayo kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike amemuita kiungo Shiza Ramadhani Kichuya katika kikosi chake  kwa ajili ya mchezo dhidi ya Lesotho na hakumuacha kando Nahodha Mbwana Alli Samatta ambaye hatacheza katika mchezo huo kutokana na kuwa na kadi mbili za njano. Samagoal kazi yake itakuwa ni kuamsha morali kwa vijana wenzake. Kikosi kizima hiki hapa

Makipa ni; Aishi Manula wa Simba SC, Aaron Kalambo wa Tanzania Prisons, Beno Kakolanya wa Yanga SC na Benedictor Tinocco wa Mtibwa Sugar zote za nyumbani.
Mabeki ni; Hassan Kessy wa Nkana FC ya Zambia, Abdi Banda wa Baroka FC ya Afrika Kusini, Shomary Kapombe, Erasto Nyoni wa Simba SC, Ally ‘Sonso’ Abdulkarim wa Lipuli FC, Kelvin Yondan, Gardiel Michael wa Yanga SC, Aggrey Morris na Abdallah Kheri wa Azam FC, zoyte za nyumbani.
Viungo ni Himid Mao wa Petrojet ya Misri, Simon Msuva wa Difaa Hassan El-Jadidi ya Morocco, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Mudathir Yahya wa Azam FC, Salum KImenya wa Tanzania Prisons, Feisal Salum wa Yanga SC, Jonas Mkude na Shiza Kichuya wa Simba SC zote za nyumbani.

Washambuliaji ni Nahodha Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji, Thomas Ulimwengu wa Al Hilal ya Sudan, Shaaban Iddi Chilunda wa CD Tenerife ya Hispania, Rashid Mandawa wa BDF XI ya Botswana, John Bocco wa Simba SC na Yahya Zayed wa Azam FC zote za nyumbani.
Kikosi hicho chini ya makocha Amunike anayesaidiwa na Mnigeria mwenzake, Emeka Amadi na mzawa Hemed Suleiman ‘Morocco’, Meneja Danny Msangi, Mtunza Vifaa Ally Ruvu na Madaktari Richard Yomba na Gilbert Kigadya kitaingia kambini nchini Afrika Kusini wiki ijayo kabla ya kwenda Lesotho siku moja kabla ya mchezo wa Novemba 18.