Rose Joseph Kamba (20) Mkaazi wa nchini Kenya amemuua mwanaye wa miezi miwili na kujiua baada ya kuibiwa Ksh.120,000 (Tsh. 2,699,345.68) katika duka la M-Pesa la Mjomba wake alipokuwa akifanya kazi

Kwa mujibu wa Mjomba wa Marehemu na Mkewe, siku ya tukio hilo walimuacha Rose nyumbani na kwenda Kanisani na waliporudi baadaye walikuta mlango umefungwa kwa ndani na waliposhindwa kufungua waliomba msaada wa Polisi

Mwili wa Rose ulikutwa ukining’inia kutoka kwenye paa la nyumba na wa mwanaye ulikutwa chumbani ukiwa umefunikwa na shuka huku damu zikitoka puani

Marehemu aliacha barua iliyosema amechukua uamuzi huo baada ya kutapeliwa fedha hizo na alipomueleza Mjomba wake, hakuamini na alidhani yeye ndiye ameiba