Serikali ya Tanzania imesema itamchukulia hatua Moses Mollel maarufu Nabii Namba Saba iwapo atashindwa kuthibitisha kauli yake kuwa ana uwezo wa kutibu wenye maambukizi ya Virusi vya Corona

Moses, mkazi wa Ngaramtoni mkoani Arusha amekuwa akijitangaza kuwa na dawa ya kutibu ugonjwa huo na kuweka mawasiliano yake kwenye mitandao

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Faustine Ndugulile ameyasema hayo katika ziara yake ya kikazi jijini Arusha. Amesema Serikali imetuma wataalamu wake kumsaka na kumhoji kama anavyo vibali vya kutoa huduma ya tiba na kujitangaza, iwapo atashindwa kuthibitisha atachukuliwa hatua kali za kisheria

Dk. Ndugulile amesema yeyote anayetoa tiba asili na mbadala lazima asajiliwe na Wizara ya Afya, dawa zake ziwe zimesajiliwa na Wizara hiyo na kusisitiza kuwa Nabii huyo pia anapaswa kuthibitisha amesajiliwa wapi na lini