Angalia Picha: Makamu wa Rais aweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa makazi ya Makamu wa Pili

Picha za michoro ya nyumba ya Makamu wa Pili wa Rais ambayo inajengwa Pagali Shehia ya Mkoroshini, Chake Chake Pemba ambapo jiwe la msingi wa ujenzi wa makazi hayo limewekwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni katika shamra shamra za kuelekea kwenye kilele cha miaka 55 ya Mapinduzi Tukufu Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi kuashiria zoezi la uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa makazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar , mwingine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Msanifu wa Majengo kutoka Ofisi ya Wakala wa Majengo Bi. Hawa Natepe mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa makazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar  katika eneo la Pagali Shehia ya Mikoroshini Chake Chake Pemba.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa makazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar  katika eneo la Pagali Shehia ya Mikoroshini Chake Chake Pemba.