Taarifa rasmi kutoka IKULU Dar es salaam ni kwamba Rais John Pombe Magufuli leo January 21 2017 amemteua Anne Kilango Malecela kuwa Mbunge kwenye Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Malecela

Anne Kilango Malecela

Mapema mwezi Machi 2016 Anne Kilango aliteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga lakini April 11 2016 Rais Magufuli alitengua uteuzi wake na katibu tawala wa mkoa huo Abdul Rashid Dachi baada ya mkoa huo kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusiana na Watumishi hewa.

Taarifa ya IKULU leo imesema baada ya Anne Kilango kuteuliwa, ataapishwa kwa mujibu wa taratibu za bunge.