Anusurika kufa baada ya kutumbukia kisimani Tunguu

Mtu mmoja ametambulika kwa jina la Neema Lucas Shija (19) amenusurika kufa baada ya kuteleza na kutumbukia kisimani wakati akichota maji kwa matumizi ya Nyumbani. 

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kamishna Msaidizi Muandamizi wa Polisi Suleiman Hassan Suleiman amesema tukio hilo limetokea leo Januari 03, 2019 majira ya saa 7 na dakika 10 mchana huko Kombeni Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa Wa Kusini Unguja.

Kamanda Suleiman ameeleza tukio hilo la kutumbukia kisimani kwa bahati mbaya wakati akichota maji kwa ajili ya maumizi Yya Nyumbani na hatimae ameteleza na kuingia kisimani na wananchi wamemtoa na kumuwahisha hospital ya Mnazi Mmoja kwa ajili Ya Matibabu.

Majeruhi huyo amelazwa hospital ya Mnazi Mmoja na hali yake sio nzuri.

Kamanda Suleiman ametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari katika harakati zao za matumizi ya nyumbani kwani visima hivi vya kienyeji vinahitaji umakini wa hali ya juu ili kuweza kuepuka ajali ambazo zinaweza kuepukika ikiwemo hali ya utelezi ambayo inaweza kuleta athari Kubwa.

Rauhiya Mussa Shaaban