Ali Vuai Ali mwenye umri wa miaka 36 amechezea kipigo baada ya kufumaniwa na mke wa mtu huko Kijiji cha Pete Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja .

Akithibitishs kutokea kwa tukio hilo Sheha wa Shehia hiyo Zakia Mbaraka Haji amekiri kupokea taarifa hiyo ya kumanizi kutoka kwa dada aliefumaniwa na ndipo alipompa taarifa mjumbe wake na  kuenda katika eneo hilo kwa haraka ili kuweza kusimamisha hali ya kipingo kilichofanywa kutoka mume wa mke.

Aidha Sheha huyo amewataka wananchi kuacha tabia ya kutumia sheria mikononi mwao na baadala yake panapotokea kitu chochote kufikisha kwa viongozi wa shehia ili kuweza kuchukuliwa hatua za kisheria.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa huo Suleiman Hassan Suleiman amesema tukio hilo limetokea siku ya tarehe 10-03 -2020 majira ya 6:30 usiku huko Kijiji cha Pete ambapo Mtuhumiwa huyo yupo chini ya ulinzi kwa hatua za kisheria.

 Rauhiya Mussa