Kijana mwenye umri wa miaka 27 Mkaazi wa Karakana aliyejulikana kwa jina la Khatibu Iddi Chumu amefariki dunia baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana kwa tuhuma za wizi wa simu huko Karakana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Awadhi Juma Haji amesema tukio hilo la kushambuliwa kijana huyo limetokea tarehe 27-02-2020 majira ya saa 4:00 Asubuhi huko Karakana.

Ameongeza kusema kuwa marehemu ameshambuliwa sehemu mbali mbali za mwili wake na amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mnazi Mmoja .

Sambamba na hayo Kamanda Awadhi amesema jeshi la polisi mkoa wa mjini linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili waweze kuwakamata kwa wale waliohusika na shambulio hilo.

Rauhiya Mussa Shaaban