Wizara ya afya maendeleo ya jamii  jinsia wazee na watoto imesema kuwa asilimia 40 ya wanawake nchini wenye miaka 15 hadi 19 wameripotiwa kufanyiwa ukatili wa kimwili huku asilimia 17 ya wanawake wenye miaka 15 hadi 49 wakifanyiwa ukatili wa kingono.

Akizungumza Mkurugenzi msaidizi wa masuala ya Watoto Bwana Sebastian Kitiku amesema takwimu hizo ni wale ambao wameripoti lakini wengine wananyamaza kimya bila kutoa taraifa wanapofanyiwa ukatili.

Bwana Kitiku amesema kuwa nusu ya wanawake waliokwisha kuolewa asilimia 85 wamefanyiwa ukatili wa kimwili na asilimia 39 ukatili wa kiakili ambapo wanaofanya hayo ni wenza wao wa karibu na kiwango hicho ni kikubwa.

””Kina mama wanafanyiwa sana ukatili na ukatili wa kimwili unaoongoza sana,vipigo kwa kila wanawake 100 waliolewa 39 wanapigwa ,wanajeruhiwa miili na wengine kuathirika kisaikolojia ni wangapi sasa wanafanyiwa ukatili huo na wanamua kuficha siri za wanaume zao” Amesema Kitiku

Hata hivyo ameongeza kuwa asilimia 54 ya wanawake ambao wamefanyiwa vitendo vya ukatili wameweza kupata msaada kwa kwenda katika matibabu,kwenye Sheria pamoja na polisi huku wengine wakiamua kukaa nyumbani na kuendelea kupata maumivu.

””Bahati mbaya sana inaweza inasababishwa na milolongo ya kuzipata zile huduma,jamii yetu inafikiria kwamba ili upate huduma ya afya ukifanyiwa ukatili kwa mfano umedhuriwa mwili wako kwa mfano ni lazima uende polisi kupata PF3 lakini kumbe mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa au mtendaji anaweza kukuandikia barua ukapate huduma katika hospitali iliyoko karibu nawewe””Amesema Bwana Kitiku

Amesisitiza kuwa ni vema waandishi wa habari  kuendelea kutoa elimu katika jamii kuhusu ukatili wa kijinsia kwasababu wengi wao hawajui jinsi taratibu za kusaidiwa pale wanapopata matatizo hayo hasa kwa watu wao wa karibu.