Afisa wa Polisi wa kituo cha Bunamwaya, nchini Uganda, Konstebo Ben Ojilong amempiga risasi Askari mwenzake, Koplo Alex Opito na mtu mmoja wa ulinzi shirikishi na kisha kujiua kwa risasi

Makamu wa Msemaji wa Jeshi la Polisi, Ndugu Luke Owoyesigyire, amesema tukio lilitokea baada ya kugombana muda mrefu kati ya maafisa hao juu ya namna ya kuendelea na kesi waliyokuwa wanaisimamia

Uchunguzi wa awali ulionesha kwamba Ojilong alimpiga risasi nyingi Opito. Askari wa ulinzi shirikishi alipigwa risasi wakati akipita na kujeruhiwa, alifariki dunia akiwa hospitalini akipatiwa matibabu

Owoyesigyire amesema Polisi wameanza kulichunguza tukio hilo na miili ya marehemu ipo katika mochwari ya mji kusubiria kufanyiwa uchunguzi zaidi