Saidi Ali Omar mwenye umri wa miaka 23 mkaazi wa Mtomchanga ameshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kumchoma kisu kijana aliefahamika kwa jina la Sheha Gora Juma.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Hasina Ramadhan Tawfik amesema majira ya saa 10 usiku Mtuhumiwa Saidi Ali Omar alimshambulia Sheha Gora Juma mwenye umri wa miaka 23 alimchoma kisu ubavuni upande wa kushoto kwa kumkuta na ndizi inayosadikiwa kuwa ya wizi huko Mtomchanga Wilaya ya Kaskazini B Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Kamanda Hasina amefahamisha kuwa niwajibu kwa kila raia linapotokezea jambo kamahilo nivizuri kufuata taratibu za kisheria nasio kujichukulia sheria mikononi mwao.

Hadi sasa mtuhumiwa huyo yupo chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja.