Wiki ya vijana kutana na mjasiriamali kijana aliebobea kwenye ujasiriamali na kuwa msaada kwa wengine

 Fursa za ajira zipo mikononi mwako endapo utaitumia vizuri akili na maarifa uliyojaaliwa na Muumba wako.

Wapo baadhi ya watu katika jamii wanashindwa ni kujua jinsi ya kuzitumia akili zao ilikutambua kitu muhimu cha kufanya, lakini ‘’fikiri ndio utende ‘’nimsemo wa wahenga.

Katika makala hii tutaona watu wanaopata  mafanikio makubwa kwa  kuamini na kutumia msemo huu na kuufanyia kazi ipaswavyo na sasa unawafaidisha  kwa kila hali kwa kutuliza akili zao.

Abla Mohamed  Baraka mkaazi wa Muembe ladu mwenye umri wa miaka (23)ni mmoja ya wasichana waliopata mafanikio  na kuzitumia akili zake kwa kutafakari  na hatimae kaweza kujiajiri  kwa kuanzisha shughuli za ujasirimali  .

  ‘’Nimeona wasomi ni wengi sana nchini na kila mmoja anataka kazi ya kuajiriwa na serikali jambo hili limenifanya nikae chini na kutafakari kiundani kitugani nifanye’’ amenza kwa kusimulia Abla Mohamed ambae ni mjasiriamali kijana.

Amesema Abla baada ya kupata jibu alianzisha kampeni yake anayoiita ‘’Mwanamke chakarika’’ambayo dhamira yake ni kumjenga mwanamke kiuchumi pia inajumuisha masuala ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto.

  ‘’Baada ya kupanga kampeni yangu ya mwanamke chakarika nikaanza shughuli  za ujasiriamali kwa kutengeneza  bidhaa  ndogo ndogo ‘’ amesema Abla.

Aidha Abla alisema  alikua hana elimu ya ujasiria mali lakini alifanya kazi kwa  bidii na matumaini baadae kupatiwa mafunzo ya  ujasiraamali  chini ya Wizara ya Biashara na Viwanda na Masoko Zanzibar imeweza kumsadia kwenye shughuli zake za kila siku  katika maisha.

Amesema  amepata mafunzo ya kutosha na anazalisha bidhaa mbali mbali ambazo zinatumiwa sana na jamii katika maisha ya kila siku, hivyo imempa mafanikio makubwa.

Amesema miongoni mwa bidhaa hizo ni kama vile marha pilipili,achari,sabuni ,dawa za kusafishia vyoo,kachumbari ya embe ,kachumbari ya mbirimbi ,kashata za njugu, choklati ,ubuyu,visheti ,ufuta na bidhaa nyengine .

Hata hivyo Abla amesema bidhaa zake zimesajiliwa na zinajulikana kama ‘’MARHA PRODUCTS ‘’na anaamini atafikia mafanikio makubwa zaidi kwa vile bado anampango wa kuengeza mtaji wa kuzalisha.

‘’ Kwa sasa nashukuru nimepata elimu ya ujasiriamali  pia natoa  mafunzo hayo ya ujasiria mali kwa wanajamii na sasa watu 160 nishawapatia mafunzo , na 75 wamefaidika na mafunzo hayo ‘’amesema  Abla Mohamed.

Hata hivyo amesema japokua kampeni yake ni mwanamke chakarika lakini hachagui jinsia anatoa mafunzo hayo kwa mtu yeyote ambaye anahitaji mafunzo kwa kuwa changamoto za maisha zinamkumba kila mmoja katika jamii hazizangatii jinsia ya mtu.

Elimu si ile tu ambayo mtu hupata darasani hata mafunzo na semina ni sehemu ya taaluma ambayo mtu ataitumia kwa malengo mazuri basi nivizuri kufanikiwa bila ya hata kutaka kujingeza zaidi wimbi la wasomi limekuwa kubwa sana visiwa vya Zanzibar lakini Abla Mohamed msichana aliehetimu kidato cha nne lakini amekuwa na msaada mkubwa katika jamii yake.

Abla Mohamed amesema kwa sasa japokua anazalisha bidhaa kidogo lakini zinamsaidia na anajitegemea mwenyewe kupitia elimu hiyo alopata na bidhaa zake zinamsaidia kupata mahitaji yake muhimu bila wasi wasi.

Pia amesema Abla Mohamed japokua bado ni mjasiria mali mdogo lakini ameshashiriki kongamano za kibiashara katika sehemu mbali mbali kama vile Maisara 7-7 day ,Dodoma 8-8day ,Arusha ,Mwanza na Dar es salam kwa ajili ya kutangaza  biashara zake .

Mitandao ya kijamii imekua ni nguvu kubwa kwa wafanyabiashara katika kutangaza biashara zao kwani huwafikia watu wengi katika jamii kwa asilimia ya wengi hutumia mitandao hii kama vile Whastup, Faceebok,Instagram na Twiter.

Abla amesema anatumia mitandao ya kijamii kama vile Facebok na Whastup kwa kutangaza bidhaa zake na kuzipeleka bidhaa zake kwenye maduka ya jumla na rejareja kama njia moja wapo ya kutangaza bidhaa hizo ambazo huzalisha kwa mikono yake na akili yake .

Mbali na hayo amesema japokua anajitegemea mwenyewe lakini zipo changamoto zinazo mzunguka kama kutopata msaada kwa jumuia na taasisi yoyote mpaka sasa licha ya jitihada anazofanya kuhakikisha siku moja kupata msaada kundeleza ujasirimali na kuwasaidia watu katika jamii yake.

Pia kutopata eneo maalum la biashara na matatizo ya kifedha pamoja na ushirikiano mdogo kwa wanawake wenzake na wengine hukata tamaa hatimae wengi huanguka kiuchumi.

Amesema Abla anatoa ushauri kwa wanajamii kwa kufanya kazi kwa bidii ilikuleta maendeleo ya kiuchumi katika nchi yetu ili tufikie malengo ya Taifa hili.

Pia ameendelea kutoa ushauri kwa wanawake kwa kujiajiri wenyewe bila kupoteza matumaini kwani wanaweza na wataweza kuepuka unyanyasaji wa wanawake endapo wataweza kujiajiri wenyewe.

Hata hivyo Abla ametoa ushauri kwa serekali wawatizame kwa jicho la tatu wajasiriamali wadogo wadogo kwa kuwapatia misaada ya elimu, kifedha pamoja na vifaa ili kuwaendeleza wanawake kiuchumi.

Kwau pande wake Saida Ali Hassan mkaazi wa Muembe shauri amesema kitendo cha kujiingiza kwenye shughuli za ujasiria mali zinampa mafanikio kwa sasa.

 ‘’ Baada ya kuona tatizo la ajira ni gumu japokua elimu yangu ni shahada ya kwanza (Degree) nikaamua kujiingiza kwenye ujasiria mali ili niepukane na tatizo la ajira na kutegemea wazazi kila siku’’amesema Saida.

Amesema saida ameweza kufanya kila njia ilikupata elimu ya ujasiria mali na ameshapata elimu hiyo kwa mwanadada Abla ambae ndie alompatia mafuzo hayo ya kutengeneza bidhaa mbali mbali.

Amesema Saida amefaidika kwani amepata mafunzo ya ujasiria mali na kwa sasa anauwezo wa kuzalisha bidhaa kama udi ,sabuni za vipande na za maji ,dawa za kusafishia ,mafuta ya mgando na nyenginezo .

Amesema Saida kwa sasa bidhaa anazozalisha kwa wingi ni udi na sabuni lakini anampango wa kuzalisha kwa wingi na kuanzisha kikundi chake ili akuze mtaji na kuwasaidia wengine amesema japokua bado ni mjasiriamali mdogo lakini anapata mahitaji yake ya msingi na bila kumtegemea mtu yoyote .

Saida ameelezea tena kwa kusema japokua anapata faida lakini kwa vile bado anazalisha vitu vichache anakumbwa na changamoto nyingi zikiwemo uhaba wa mtaji  Pia amesema Saida kutokuwepo kwa mashirikiano mazuri kwa washirika wa ujasiriamali ni moja ya changamoto inayo muathiri .

Saida ametoa ushauri kwa wanawake na vijana kwa jumla kujiingiza kwenye shughuli za ujisiriamali ilikuepukana na tatizo la ajira katika jamii zetu, pia Saida ametoa ushauri kwa serekali kuwapa msaada wale walio pata mafunzo ili waweze kuanzisha miradi yao wenyewe.

Nae Fat-hia  Abdulihamid Ali mkaazi wa mikunguni  mwenye umri wa miaka 19 amehitimu masomo yake mwaka 2016 amesema ujasiria mali ni mkombozi kwa mwanamke na inamfanya kuweza  kujitegemea mwenyewe.

  ‘’kitendo cha kushindwa  kujiendeleza na masomo imenifanya nijishirikishe kwenye ujasiria mali ili nipate mahitaji yangu ‘’amesema Fat-hia.

Amesema baada ya kukosa kuendelea na masomo hapo alianza kutafuta elimu ya ujasiria mali kila sehemu na ameshapata elimu hiyo na kwa sasa anauwezo mzuri wa kuzalisha bidhaa nyingi , aidha  ameendelea kusema ujasiriamali umempa fursa ya kijiajiri mwenyewe kwa kutengeneza sabuni, mafuta na  bidhaa nyengine pia kuweza kupata mahitaji ya lazima .

Hata hivyo amesema ujasiria mali umumempa matumaini na kujiona kuwa mwanamke anaweza kama mwanaume na  kuzalisha bidhaa nyingi endapo atafanya bidii.

Fat-hia amesema kunauwezekano ambapo utaweka nia na mwanzo unanza na kidogo na baadae unakuza mtaji baada ya kujitangaza na kujilikana na jamii.

Pia amesema Fat-hia kila chenyefaida hakikosi hasara hivyo amesema anapata vikwazo vingi lakini kama mjasiriamali hanabudi kupambana na changamoto iliaweze kufikia mafanikio anayo tarajia.

Amesema miongoni mwa changamoto ni pamoja na kuzarauliwa ,kushangaliwa ,uhaba wa kifedha na kukosasa mashirikiano na misaada .

Fat-hia amesema changamoto hizo bado anapambana nazo na kuengeza bidii ili afikie mafanikio alio jiwekea kwa kufikia mjasiria mali mkubwa.

Hata hivyo ametoa ushauri kwa wanawake wenzake kwa wakae na kufikiria cha kufanya pia wafanye kazi tofauti kwa kuwa na matumaini  mafanikio kwa moyo mkunjufu.

Pia ametoa ushauri kwa serekali na taasisisi binafsi kutoa misaada ili waweze kuwanyanyua wanawake kiuchumi na kupunguza unyanyasaji wa kijinsia katika jamii ambao umekuwa ndio kero kubwa katika jamii yetu ya Zanzibar.

Mwanamke akiwezeshwa jamii nzima imeweza kujiwezesha kwa kuwa nafasi kubwa na majukumu aliyonayo mwanamke ni kuweza kusaidiwa ili ipate mafanikio na kuweza kujikomboa kiuchumi kwani wa ndio uti wa mgongo wa Familia zetu .

Hata hivyo mwanamke anauwezo mkubwa wa kijishughulisha katika kila kazi ya kijamii ili kupata mahitaji yake bila kumtegemea mwanaume ,kituambacho kinampa mwanamke kuishi bila wasi wasi  na kuepukana na vishawishi katika jamii.