Shirikisho la mchezo wa mpira wa miguu visiwani Zanzibar limeandaa mchezo wa hisani kati ya Azam FC dhidi ya Mtibwa Sugar kama sehemu ya kumuenzi kiungo za zamani wa timu hizo Ibrahim Jeba aliyefariki dunia mwaka huu.

Mchezo huo wa hisani unaolenga kukusanya pesa na kuchangia familia ya mchezaji huyo, utapigwa Desemba 9 2019 katika uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.

Siku ya mchezo huo zitauzwa jezi za Azam FC na Mtibwa Sugar zilizoandikwa jina la mchezaji huyo.

Jeba enzi za uhai wake aliwahi kuzichezea timu hizo mbili kwa nyakati mbili tofauti. Alifariki Dunia Septemba 19 2019 katika hospitali ya Mnazi Mmoja Unguja Zanzibar na kuzikwa Septemba 20.